STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 6, 2014

Panga pangua makamanda wa Polisi hii hapa, Shilogile dah!

IGP Mangu akizungumza kwenye mikutano ya jeshi la Polisi
INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu, amemhamisha kazi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Faustine Shilogile.

Shilogile amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam huku nafasi yake ikichukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paul.

Kwa mujibu wa IGP Mangu, uhamisho huo ni sehemu ya utendaji wa kawaida ndani ya Jeshi la Polisi na kwamba umezingatia kanuni, taratibu na miongozo ya jeshi hilo.

Katika uhamisho huo uliowagusa baadhi ya makamanda wa mikoa hapa nchini ambapo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustine Olomi naye amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.

Katika uhamisho huo nafasi ya Kamanda Olomi imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Juma Saad Khamis, aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aidha, uhamisho huo umemgusa pia Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Joseph Konyo, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mwanza, anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Haji Khamis Haji aliyekuwa Ghasia Kuu Zanzibar anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba.
Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment