Kikosi
cha Kuzima Moto kikizima moto nyumba jirani na Hospital ya TMJ iliyopo
Mikocheni Dar es Salaam muda huu na watu kudhani kuwa iliyokuwa ikiungua
ni hospitali.
Wagonjwa wakitolewa nje na manesi wa Hospital ya TMJ baada ya nyumba jirani kuwaka moto.
Hospital ya TMJ iliyopo Mikocheni Dar es Salaam ilizushiwa kuwaka
moto baada ya nyumba jirani kulipuka moto, hali iliyosababisha hekaheka
kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo ya kuwatoa nje wagonjwa kwa tahadhari.
Tahadhari hiyo ilichukuliwa kutokana na wasiwasi kuwa moto huo
ungeweza kuvuka na kuingia hospitali lakini ulidhibitiwa na kikosi cha
zima moto na kuishia katika nyumba hiyo ya jirani.
Picha: Haruni Sanchawa na Makongoro Oging
No comments:
Post a Comment