STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 6, 2014

Side Boy Mnyamwezi hana mpango na albamu

Side Boy katika pozi tofauti
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Said Saleh 'Side Boy Mnyamwezi' amaesema hana mpango wa kutoa albamu kama alivyowahi kufanya siku za nyuma badala yake ataendelea kuangusha 'singo' moja moja baada ya kutofaidika na albamu zake za awali.
Akizungumza na MICHARAZO, Side aliyeachia wimbo mpya wa 'Usimdharau Usiyemjua' aliyoimba na Ney wa Mitego, alisema kutokana na unyonyaji na uharamia wanaofanyiwa wasanii kupitia mauzo ya albamu, jambo ambalo hate yeye limemkuta ameamua kutotoa tena albamu kama alivyokuwa amepanga.
Side Boy, alisema ni bora kutoa wimbo mmoja mmoja na video yake kuliko kutoa albamu inayogharimu mamilioni ya fedha na kuishia kuambulia patupu.
"Sina mpango wa kutoa albamu kama nilivyowahi kufanya siku za nyuma, kwa sasa nitakuwa natoa 'singo' tu kwa lengo la kujitengenezea nafasi ya kuvuna fedha na kupata mialiko ya maonyesho," alisema.
Side Boy siyo msanii wa kwanza kutoa msimamo huo kwani, kauli kama hiyo iliwahi kutolewa na wasanii mbalimbali kutokana na kinachoelezwa wizi na unyonyaji unaowafanya wasanii wasinufaike na jasho lao

No comments:

Post a Comment