STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 22, 2013

Tevez akizidi kung'ara Italia, Inter yaua 7-0

Carlos Tevez
Tevez (10) akishangilia bao lake na wachezaji wenzake wa Juventus
 MSHAMBULIAJI nyota wa Argentina, Carlos Tevez ameendelea kung'ara kwenye Seria A baada ya leo kuisaidia Juventus kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Hellas Verona, huku mabingwa wa zamani wa Ulaya, Inter Milan ikipata ushindi wa kishindo wa mabao 7-0 ugenini dhidi ya Sassuolo.
Tevez aliyetua kwa mabingwa hao watetezi wa Seria A akitokea Manchester City, aliifungia Juventus bao la kusawazisha dakika ya 40 baada ya  wageni wao kutangulia kwa bao lililofungwa na Cacciatore kabla ya Fernando Lliorente kufunga bao la pili na la ushindi sekundu chache kabla ya mapumziko.
Nayo Inter Milan ikiwa ugenini iliisulubu Sassuolo mabao 7-0, wafungaji wake wakiwa ni Palacio aliyefunga dakika ya 7, Taide dakika ya 23 na Pucino wa Sassuolo aliyejifunga dakika ya 33 na hadi mapumziko washindi walikuwa mbele kwa magoli 3-0.
Mabao mengine yalifungwa na Alvarez, Diego Milito aliyefunga mawili na Cambiasso.
Katika mechi nyingine za ligi hiuyo Fiorentina ilipata ushindi ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya Atalanta, Bologna kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Torino, As Roma kuizima lazio mabao 2-0 na Catania na Parma kushindwa kutambiana na muda mchache ujao itashuhudiwa pambano la kukata na mundu klati ya Ac Milan itakayoialika Napoli uwanja wa San Siro.















No comments:

Post a Comment