STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, July 12, 2013

Man City yapania kumnasa Ronaldo

http://i2.mirror.co.uk/incoming/article1867031.ece/ALTERNATES/s615/Cristiano-Ronaldo-1867031.jpg
Ronaldo
MANCHESTER, England
MANCHESTER City wameamua kuvunja benki kwa nia ya kumshawishi mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo atue katika uwanja wa Etihad katika kipindi hiki cha usajili.
Na wameiambia kambi ya Ronaldo kwamba wamejiandaa kuipiku ofa kutoka kwa Manchester United, jambo linalomaanisha kwamba wako tayari kumlipa mshahara wa zaidi ya paundi 300,000 (Sh. milioni 709) kwa wiki.
Man U wametumia miezi mitano iliyopita kujaribu kuandaa dili la kumrejesha Old Trafford nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, na Ronaldo mwenyewe ameshaonyesha kwamba bado timu hiyo iko moyoni mwake.
Man City wanatambua kuwa jambo hilo ni kiunzi kigumu kuruka, lakini mkurugenzi mtendaji wao Ferran Soriano na mkurugenzi wa soka Txiki Begiristain wote wamewaambia mawakala wa mchezaji huyo kwamba wako 'siriasi' sana na uhamisho huo.
Na wameweka wazi kwamba kama Real watakuwa tayari kumuachia Mreno huyo aondoke, watafanya kila liwezekanalo kuwapiku mahasimu wao Man U.
Mwenyekiti wa Man City, Sheik Mansur ameweka wazi kwa Soriano kwamba kama Ronaldo ataingia sokoni, City ni lazima wafanye chochote kinachowezekana kuhakikisha wanamsajili.
Ronaldo amebakisha miaka miwili katika mkataba wake Hispania, lakini licha ya kusema hadharani kwamba anakaribia kusaini mkataba mpya, Real bado hawajampa ofa yoyote ya mkataba mpya.
Jambo hilo linawaongezea matumaini Man U kwamba wanaweza kumnasa, ingawa mipango hiyo mipya ya Man City inaleta presha mpya Old Trafford.
PSG ndiyo klabu pekee ambaye kufikia sasa iliwasilisha ofa ya paundi milioni 55 ambayo Real waliikataa.
Klabu hiyo ya Ufaransa inajiandaa kumlipa pesa nyingi zaidi, lakini Ronaldo anafahamika kwamba anavutiwa zaidi kurejea Uingereza kama ataondoka Bernabeu.
 

No comments:

Post a Comment