KLABU za Manchester City
ya Uingereza na Paris Saint-Germain ya Ufaransa watakabiliwa na adhabu
baada ya kukiuka maadili ya sheria ya matumizi ya fedha ya Shirikisho la
Soka barani Ulaya-UEFA.
Mbali na hao vilabu vingine vipatavyo 20
vinaaminika kukutwa na hatia ya kuvunja sheria hiyo.
UEFA itatoa ofa
maalumu kwa vilabu hivyo vilivyokiuka sheria hiyo kuelekea katika
mkutano wao utakaofanyika Alhamisi.
Adhabu kubwa ambayo ni timu husika
kuenguliwa katika michuano ya Ulaya haitarajiwi kuwepo ingawa pia
hawakuweka wazi ni adhabu zipi zitaazotolewa kwa timu hizo.
No comments:
Post a Comment