Dani Alves aliebaguliwa Hispania na shabiki wa Villarreal |
Rais wa Brazil Dilma akiwa na Rais wa FIFA |
RAIS Dilma Rousseff, amesifu kitendo cha mchezaji wa kimataifa wa
Brazil, na Barcelona Dani Alves kutokana na tukio la ubaguzi wa rangi
wakati wa mechi ya ligi kuu ya Uhispania, La Liga kati ya Barcelona na
Villareal .
Mchezaji huyo wa Barcelona aliokota ndizi aliyokuwa ametupiwa na kuila kabla ya kuitupa na kuendelea na mchezo.
Bi
Rousseff aliandika katika mtandao wake wa twitter kuwa Dani Alves
alionyesha ujasiri wa kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika kandanda na
kuwa ni tukio la kuigwa .
Klabu ya Villarreal inasema
kuwa imempiga marufuku mwanaume ambaye alitupa ndizi hiyo uwanjani na
kuwa hatohudhuria mechi zote za nyumbani za klabu hiyo maishani.
Mamia
ya watu na wachezaji maarufu duniani wameonyesha upendo wao kwa
mchezaji huyo kwa kuweka picha zao kwenye mitandao wa kijamii wakila
ndizi.
Mchezaji wa Manchester City Sergio Aguero alipachika picha akila ndizi sawa na nyota ya soka ya wanawake Marta .
Wengine ni Luiz Suarez wa Liverpool,Oscar, David Luiz na Willian wote wa Chelsea .
Rais
wa Fifa sepp Blatter ameongezea sauti yake katika tukio la hivi punde
akisema ni vibaya kwa dhulma hizo kuendelea katika karne hii.
BBC
No comments:
Post a Comment