STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 29, 2014

Jahazi la timu ya Babi lazidi kuzama Malaysia

Kikosi cha UiTM anayoichezea Abdi Kassim (wa kwanza kulia mbele)
JAHAZI la timu ya UiTM anayoichezea kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' limezidi kuzama kwenye Ligi Kuu ya nchini Malaysia baada ya jana kufungwa kwa mara ya pili mfululizo.
UiTM iliyokuwa ugenini, ilikumbana na kipigo cha bao 1-0 toka kwa wenyeji wao Negeri Sembilan,  waliowafuata kwenye uwanja Tuanku Abdulrahaman, mjini Seremban ikiwa ni siku chache tangu idunguliwe nyumbani kwa mabao 4-1 na Felda United.
Kipigo hicho cha jana ni cha sita katika michezo 9 iliyocheza timu hiyo na kuifanya izidi kuporomoka kwenye msimamo wa ligi hiyo ikienda nafasi ya 11, nafasi moja toka mkiani.
UiTM iliyomsajili Babi kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea KMKM imesaliwa na pointi zake 7 kutokana na kushinda mechi mbili tu na kuambulia sare moja na kupoteza mechi zilizosalia.
Timu hiyo inatarajiwa kushuka dimbani Ijumaa ijayo kwa kuvaana na Kedah kwenye uwanja wao wa nyumbani.

No comments:

Post a Comment