STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 3, 2015

Yanga yafanya kufuru yatenga fedha Ebola Cup

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/05/SAM_1702.jpg
Mwwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji ametenga kiasi cha dola 500,000 kwa ajili ya michuano ya Ebola  Cup itakayoshirikisha timu 108 za Afrika.
Katika michuano hiyo Tanzania itawakilishwa na Yanga pamoja na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Yanga, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Jonas Tibohora  alisema hatua za kuanza michuano hizo zipo kwenye hatua nzuri.
Alisema michuano hiyo imeandaliwa kwa ajili ya  kuchangisha fedha  zitakazowasaidia waafrika walioathirika na ugonjwa wa Ebola.
Alisema michuano hiyo itasimamiwa na Chama cha Soka Afrika (CAF), na kwamba kwa sasa kamati ya michuano hiyo yenye wajumbe mchanganyiko kutoka nchi wanachama wa CAF itakaa na kupanga tarehe ya michuano hiyo.
Alisema michuano hiyo itachezwa kwa mtindo wa makundi ambapo kutakuwa na makundi 16 na kila kundi litakuwa na timu kati ya nne na saba.
Alisema michuano hiyo itashirikisha timu zote kutoka Afrika ambazo ni mwanachama wa CAF ambapo kila nchi itatoa timu mbili na michuano itachezwa nyumbani na ugenini.
Alisema  kila timu zitachangia kiasi cha dola 100,000 kama ada ya ushiriki ambazo zitaingizwa moja kwa moja katika mfuko wa kusaidia waathirika hao.
"Mpango huu yatari umepitishwa na kinachofuata ni kupangwa kwa tarehe ya michuano ambapo kamati ya mashindano inayoongozwa na Mwenyekiti wake Machache Shipanda kutoka Zambia itakutana na kutoa ratiba,"alisema Tibohora.
Alisema pia mpango huo umeungwa mkona na umoja wa Afrika (AU) ambao watashirikiana kwa pamoja kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa manufaa makubwa.


No comments:

Post a Comment