STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 4, 2015

CAF yamfungia mwamuzi aliyewabeba wenyeji Afcon 2015

http://ww1.hdnux.com/photos/34/36/27/7464396/5/628x471.jpg
Refa Seechurn Rajindraparsad

https://s.yimg.com/bt/api/res/1.2/RFZ6duPBZw4ebZ6b797g2A--/YXBwaWQ9eW5ld3M7cT04NTt3PTYzMA--/http://media.zenfs.com/fr_FR/Sports/Eurosport/1405900-30114704-640-360.jpg
Polisi wakimlinda mwamuzi Rajindraparsad asipewe kichapo na wachezaji wa Tunisia baada ya kutoa penati tata kwa wenyeji dakika za lala salama
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemsimamisha mwamuzi Seechurn Rajindraparsad aliyevurunda pambano la Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya wenyeji Guinea ya Ikweta na Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) kutakiwa kuomba msahama kwa vurugu zilizofanywa na wachezaji wa nchi hiyo.
Mwamuzi huyo kutoka Mauritius alitoa penati ya utata dakika za lala salama za pambano hilo na kuwapa wenyeji bao la kusawazisha lililofanya mchezo huo kuongezewa muda wa dakika 30 na Guinea ya Ikweta kushinda kwa mabao 2-1 na kutinga nusu fainali.
Wachezaji wa Tunisia walionyeshwa kukerwa na maamuzi hayo kiasi cha askari Polisi kulazimika kumuokoa na kumlinda ili asidhuriwe.
Katika taarifa yake iliyotolewa juzi, CAF imetangaza kuondoa mwamuzi huyo kwa kuchezesha ovyo mechi hiyo na kusimamisha kwa muda wa miezi sita sambamba na kumuondoa kwenye orodha ya Caf ya waamuzi wa Daraja A kutokana na kikao cha Kamati ya waamuzi.
Mwamuzi huyo licha ya 'kubanyanga' mchezo huo ambao ulionekana wazi wenyeji wameondoshwa mashindanoni, huku TFT ikitakiwa kuomba radhi kwa vitendo vilivyofanywa na wachezaji wa timu yao ya taifa  siku ya mchezo huo.
TFT tayari imeshaadhibiwa kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 kwa utovu wa nidhamu wa wachezaji wa timu yao ya taifa na maafisa wake, ingawa CAF kupitia kamati ya Waamuzi inakiri kwamba mwamuzi wa pambano hilo alivurunda kwa kuchezesha chini ya kiwango jambo ambalo CAF haipo tayari kuona madudu kama hayo katika michuano yake.

No comments:

Post a Comment