STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 21, 2012

Aliyedai Asizikwe Atafufuka Baada ya Siku Mbili Asababisha Balaa

NewsImages/6601474.jpg
Tuesday, September 18, 2012 4:25 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Afrika Kusini ambaye alidai enzi za uhai wake kuwa atakapofariki asizikwe kwakuwa atafufuka baada ya siku mbili ameshindwa kufufuka baada ya kifo chake na maiti yake imekuwa kero kwa watu kutokana na harufu kali inayotoa.
Mwanaume huyo aliyekuwa mkazi wa Tsolo, Eastern Cape nchini Afrika Kusini aliwaagiza ndugu zake wakati wa uhai wake kuwa atakapofariki basi mwili wake usipelekwe monchwari kwakuwa atafufuka baada ya siku mbili.

Mwanaume huyo alifariki jumanne ya wiki iliyopita na ndugu zake walifuata maagizo yake kwa kuuweka mwili wake nyumbani kwake wakimsubiria arudi toka kuzimu akiwa hai tena.

Familia yake iliendelea kuutunza mwili wake huku wanajumuiya wa kanisa lake wakija kumuombea dua.

Baada ya siku mbili kupita ambazo alidai angefufuka maiti yake ilianza kuharibika na kutoa harufu kali iliyoanza kuwa kero kwa majirani.

Msemaji wa eneo hilo aliyetambulishwa kama Sizwe Kupelo aliwaambia waandishi wa habari kuwa majirani wameanza kulalamika harufu kali inayotoka kwenye nyumba yake.

"Limekuwa tatizo la kiafya sasa, watu wanaohofia kupata maambukizi", alisema Kupelo.

Timu ya maafisa wa afya na mapolisi walitarajiwa kuitembelea familia hiyo na kuishawishi iachane na mawazo ya kusubiria kufufuka kwa ndugu yao na hatimaye wauzike mwili wake kama inavyotakikana.


Nifahamishe.com    

No comments:

Post a Comment