STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 19, 2014

Maskini Arsenal yamkosa Debuchy wiki 6

http://ep.imgci.com/PICTURES/CMS/72200/72245.3.jpgIMETHIBITIKA kuwa, beki wa kulia wa Arsenal, Mathieu Debuchy atakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki sita hali inayozidi kuiweka pabaya klabu hiyo.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Debuchy atakaa nje ya uwanja kwa kipindi hicho kutokana na kuumia kwake kifundo cha mguu. 
Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye alitolewa nje kwa machela katika mchezo dhidi ya Manchester City Jumamosi iliyopita anaweza kukosekana kwa miezi mitatu kama itahitajika kufanyiwa upasuaji. 
Wenger alithibitisha hilo na kudai kuwa matokeo zaidi watayajua katika siku chache zijazo baada ya kufanyiwa vipimo zaidi kuonyesha jinsi eneo hilo lilivyoathirika. 
Calum Chambers,19 anatarajiwa kuchukua nafasi ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 katika mchezo wa kesho dhidi ya Aston Villa. 
Debuchy aliyejiunga na Arsenal akitokea Newcastle United Julai mwaka huu amecheza katika mechi zote saba za timu hiyo msimu huu ukiwemo mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City. 
Beki mwingine kinda Hector Bellerin,19 ndio aliyeingia kucheza nafasi ya upande wa kulia katika mchezo wa Jumanne waliofungwa na Borussia Dortmund kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments:

Post a Comment