STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 27, 2014

Wajasiriamali 200 wapewa mafunzo Kanda ya Ziwa

http://danalbrecht.com/wp-content/uploads/2010/04/rocks.jpgNA SULEIMAN MSUYA
ZAIDI ya Wajasiriamali 200 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa wameshiriki mafunzo ya jinsi ya kuandaa bidhaa kabla ya kuingia sokoni yaliyoandaliwa na kampuni ya Usalama Chakula na Ubora (Food Safety and Quality Consultancy Co. Limited) jijini Mwanza.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Petronella Mlowe wakati akizungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu akiwa mkoani Mwanza.
Mlowe alisema katika mafunzo hayo yaliyofanyika jana na leo jijini Mwanza yamepata mafanikio makubwa kwa kuwepo kwa mwitikio kwa wajasiriamali wakiume zaidi ya wanawake.
Alisema pamoja na mwitikio mkubwa kutoka kwa wajasiriamali amebaini kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kwa wahusika wa mafunzo hayo hasa kwenye maandalizi ya bidhaa jambo ambalo amesema kuwa ni muhimu serikali ikatumia vyombo vyake kuwajengea uwezo wajasiriamali.
“Mafunzo yamekuwa ya mafanikio makubwa sana hasa kwa wanaume wengi wamejitokeza jambo ambalo limenipa matumaini ya kuendelea na kampeni hii ambayo ina lengo la kukuza uchumi wa wa wajasiriamali wa Kitanzania”, alisema.
Mkurugenzi huyo alisema mafunzo hayo yalishirikisha wajasiriamali kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Bukoba na Geita ambapo waliomba kampuni hiyo kuendelea na mpango huo ili kuhakikisha kuwa wanapata mafanikio.
Alisema wajasiriliamali wengi ni wale ambao wanajihusisha na uuzaji wa asali, maembe, chili, pilipili na bidhaa nyingine mbalimbali ambazo zimekuwa zikiuzwa katika soko la ndani ila la nje hazipatikani.
Pia alitoa wito kwa asasi, taasisi na mashirika mengine ambayo yanajihusisha na kuelimisha kutoa elimu ya jinsi ya kuandaa bidhaa hasa katika kuweka lebo ili kuhakikisha kuwa ubora wa bidhaa unapatikana ili kuleta ushindani wa ndani na nje ya nchi.
Mlowe alisema kampuni yao itaendelea kushirikiana na wajasiriamali ambapo zoezi hilo linaendelea katika mkoa wa Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 hadi 29 mwezi huu lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanapata uelewa mzuri juu ya uandaji wa bidhaa.

No comments:

Post a Comment