STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 27, 2014

Tanzania Kwanza yaishutumu UKAWA kwa kiburi

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2014/04/Mwenyekiti-wa-Kamati-ya-Tanzania-Kwanza-ya-Nje-ya-Bunge-la-Katiba-Agustino-Matefu-alionesha-waraka-wa-Tundulisu-ambao-aliikataa-Zanzibar-kushoto-ni-Iddi-Majuto-Katibu-wa-Kamati-hiyo.jpg
Augostino Matefu (kulia)
http://udakuleo.com/wp-content/uploads/2014/04/3b83d__ukawa.jpg
Viongozi wakuu wa UKAWA wanaoshutumiwa na Tanzania Kwanza
NA SULEIMAN MSUYAWAKATI Wabunge wajumbe wa Bunge la Katiba Wanaounga Mkono Rasimu iliyotolewa na iliyokuwa Tume ya Rasimu ya Katiba wakijulikana kwa jina maarufu la (UKAWA) wakiendelea na msimamo wao wa kutorejea Bungeni Kamati ya Tanzania Kwanza imewashutumu kuwa kiburi chao kinasababishwa na wafadhili kutoka Ujerumani na Uholanzi.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Augustino Matefu wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema takribani wiki moja iliyopita alipozungumza na wanahabari alitoa siku saba za UKAWA kurejea Bungeni na kinyume cha hivyo ataweka wazi juu ya nini kinawapa kiburi wabunge hao.
Matefu alisema  vyama vya CDU na Consecutive  kupitia benki moja kubwa ya nchini Ujerumani na taasisi inayojulikana kwa jina la (KAS) wamekuwa wakiwapatia viongozi wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) fedha haramu zaidi ya bilioni 4.6 kwa lengo la kugomea bunge la katiba linaloendelea mkoani Dodoma.
“UKAWA wanapokea fedha kutoka Ujerumani ndio maana wanakataa kuingia bungeni na kama kuna mtu anabisha aende mahakamani na sisi tunaonyesha ushahidi kwani fedha hizo zimeingia katika akaunti ya Freeman Mbowe na Dk. Wilbrod  Slaa na ipo taasisi hapa nchini ndio inapokea”, alisema
Alisema vyama hivyo vya siasa vinavyosaidia UKAWA kupitia viongozi wakuu wa CHADEMA vina lengo la kuvunja amani ya nchi jambo ambalo Tanzania Kwanza hawawezi kulivumilia.
Mwenyekiti huyo alisema UKAWA kupitia akaunti ya Mbowe na Slaa mnamo tarehe 4 hadi 15 mwezi Machi waliingiziwa shilingi bilioni 1.7, mwezi Machi huo tarehe 26 mwaka huu UKAWA walipokea shilingi milioni 380 kupitia akaunti ya Mbowe.
Matefu alisema hivi majuzi Mbowe amepokea shilingi milioni 580 kwa lengo la kufadhili maandamano ambayo kwa mujibu wa Matefu yataweka nchi hatarini ambapo aliomba Watanzania kutounga mkono.
Aidha alisema hivi karibuni vyama hivyo vya Ujerumani vimeahidi kuingizia vyama vya umoja wa UKAWA shilingi bilioni 4.6 hiyo ikiwa ni baada CHADEMA kuonyesha msimamo wa kutoridhia maridhioano na chama tawala CCM kwa kile anachodai Matefu kuwa CCM itaongoza milele.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment