STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 21, 2013


TUZO ZA MUZIKI ZA KILI 2013 ZAZINDULIWA

Katikati ni Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL kulia na Godfrey Mungereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA kushoto pamoja na Maofisa wa TBL na BASATA wakifurahia jambo mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 sambamba na nembo ya tuzo hizo. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es salaam  (Picha: Executive Solutions)
Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey Mungereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager kudhamini tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards kwa miaka mingine mitano mpaka 2018 sambamba na uzinduzi wa tuzo hizo kwa mwaka 2013 huku viongozi wengine wa TBL na BASATA wakipiga makofi. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es salaam jana.(Picha: Executive Solutions)

TUZO za muziki maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zimezinduliwa jana jijini Dar es Salaam zikiwa na dhumuni kubwa la kutambua wasaniii waliopata mafanikio katika sekta ya muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

George Kavishe, Meneja wa  kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa, “Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuendelea kudhamini  tuzo hizi kwa mara ya 12 sasa lengo likiwa kukuza muziki nchini Tanzania. Mchakato wa kuwapata wanamuziki bora wa mwaka unaanza leo na utamalizika tarehe 8 Juni ambapo tutakuwa na hafla ya usiku maalum wa kwa ajili ya kutangaza washindi.”

Alisema Kilimanjaro Premium  Lager imejizatiti kuendeleza tasnia ya muziki Tanzania kwa kutambua na kuwapa tuzo wasanii wenye vipaji. ‘Tunataka  wanamuziki  wetu wajisikie wanathaminiwa na kutambuliwa kwa kazi nzuri wanayoifanya  vile vile tunataka Watanzania  waweze kuthamini muziki wa nyumbani na kutambua mchango wa wanamuziki katika kuleta maendeleo ya uchumi katika nchi.

‘’Kilimanjaro Premium Lager inajivunia  kuwa sehemu ya tuzo hizi na ni matumaini yetu kua mwaka huu tukio hili litakua kubwa na zuri zaidi’’

‘’Pia tuna furaha kutangaza  kwamba BASATA imetupatia leseni ya kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa kipindi cha miaka mingine mitano. Kusainiwa kwa mkataba mpya na BASATA ni uthibitisho wa azma kubwa tuliyonayo katika kuendeleza muziki wa Tanzania. Mkataba huu utaifanya Kilimanjaro Premium Lager kuwa mdhamini wa tuzo hizi mpaka mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment