STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 21, 2013

Kamanda Andengenye kuzishuhudia Golden Bush v Wahenga Pasaka

Kamanda Thobias Andengenye

KAMANDA wa zamani wa Polisi wa Mikoa ya Morogoro na Arusha ambaye kwa sasa amehamishiwa Makao Makuu jijini Dar es Salaam, Afande Thobias Andengenye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la soka la 'wazee' kati ya Golden Bush Veterani na Wahenga Fc.
Pambano la wapinzani hao wa jadi linatarajiwa kufanyika siku ya Pasaka kwenye uwanja wa TP Afrika, Sinza, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mlezi na Msemaji wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico', Kamanda Andengenye amethibitisha kuwa mgeni rasmi wa pambano hilo litakalochezwa saa 10 jioni siku hiyo ya Pasaka.
Ticotico, alisema walithibitishwa na kamanda huyo jana na hivyo kupata faraja kubwa ya kuona kamanda huyo kulishuhudia pambano hilo la wapinzani hao wa jadi.
Macocha Mayay wa  Wahenga, akiwaburuza wachezaji wa Golden Bush walipokutana mara ya mwisho Janurai 12, 2013 na Golden Bush kushinda mabao 4-3 na kulipa kisasi cha kipigo kama hicho walichopewa na wapinzani wao Desemba 31, 2012.

"Kamanda Thobias Andengenye ametuthibitishia kuwa mgeni rasmi katika pambano letu dhidi ya Wahenga litakalochezwa siku ya Pasaka," alisema Ticotico.
Ticotico alisema katika kujiweka fiti zaidi kabla ya kuvaana na wapinzani wao hao Jumamosi wanatarajia kushuka dimbani tena kuuvaana na Kijitinyama Veterani katika uwanja wa Bora.
"Katika kujiweka vyema zaidi kabla ya kuwaangushia kipigo Wahenga, Jumamosi tutacheza mechi ya mwisho ya kujipima nguvu dhidi ya Kijitonyama Veterani pale kwenye uwanja wa Bora," alisema Ticotico.
Wahenga inayotambia wachezaji kadhaa nyota kama akina Mengi Matunda, Yona Babadimo na wengine na Golden Bush yenye nyota wa zamani wa Simba na Yanga, kama akina said Swedi, Yahya Issa, Wisdom Ndlovu, Athuman Machuppa na wengine hilo litakuwa pambano lao la nne baada ya awali kuvaana mara tatu na kutambiana mara moja moja na mechi yao nyingine kutoka sare ya bao 1-1.

No comments:

Post a Comment