STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 27, 2014

Arsenal katika mtihani mzito leo Ulaya

WAKATI kiungo wake mahiri, Jack Wilshere akiamini kuwa sare ya 2-2 waliyopata na Everton mwishoni mwa wiki itawasaidia kuwapoa morali wa kufanya vyema katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Arsenal ina mtihani mgumu leo.
Klabu hiyo ya meneja Arsene Wenger inaikaribisha Besiktas ya Uturuki katika mechi ya marudiano ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ze Gunnerz wakihitaji ushindi ili kuingia kwenye makundi.
Katika mechi ya mkondo wa kwanza timu hizo zilipokutana mjini Instabul, zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bila magoli, huku Arsenal ikimpoteza nyota wake kwa kupewa kadi mbili za njano na kufuatia nyekundu.
Walshere anaamini Arsenal wapo poa baada ya kufanikiwa kutoka nyuma kwa kufungwa mabao 2-0 na kufanikiwa kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton Jumamosi iliyopita. 
Akihojiwa Wilshere amesema alama waliyopata dhidi ya everton ilikuwa ni muhimu kwani inawapa nguvu kwa ajili ya mchezo wao wa leo ambapo sare ya aina yoyote inaweza kuwaondoa mashindano ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka mingi kwa vijana hao wa Emirates.

No comments:

Post a Comment