STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 10, 2016

Tetesi za usajili majuu zipo hivi

http://i2.walesonline.co.uk/incoming/article6494703.ece/ALTERNATES/s615/1Gareth-Bale.jpgDIRISHA la usajili kwa mwezi Januari lipo wazi na klabu kadhaa zimeanza kuchangamkia kwa kunyakua nyota mbalimbali, huku tetesi nyingine zikizidi kuenea kila uchao.
Straika wa Real Madrid, Gareth Bale anatarajiwa kukataa maombi ya kutoka Manchester United na Chelsea kufuatia nyota huyo wa kimataifa wa Wales kutaka kuendelea kubakia Santiago Bernabeu. Pia inaelezwa kuwa Klabu ya Manchester United inaripotiwa kujipanga kumchukua meneja wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino kama mbadala wa Louis van Gaal, huku meneja wa Paris Saint-Germain Laurent Blanc naye akitajwa kufikiriwa katika nafasi hiyo. Hii ni kwa mujibu wa Sunday Mirror. 
Kwingineko klabu ya Tottenham Hotspurs inajipanga kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy kwa mkopo majira haya ya kiangazi, huku Manchester United inataka kitita cha paundi milioni 24 kwa ajili ya Marouane Fellaini lakini hawatakubali kiungo huyo kuondoka kwa mkopo. Pia klabu hiyo ya Manchester United inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Mainz Yoshinori Muto kwa kitita cha paundi milioni 12 hii ni kwa mujibu wa Sunday Mirror.
The Suna lenyewe limeeleza kuwa Klabu ya Manchester City imeingia katika kinyang’anyiro cha paundi milioni 80 na Real Madrid na Paris Saint-Germain kama Eden Hazard ataamua kuondoka Chelsea kipindi hiki cha majira ya kiangazi, huku Chelsea nayo ikidaiwa kuwa inamuwinda meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ili aweze kuwa mbadala wa Guus Hiddink pindi atakapomaliza muda wake mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment