STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 22, 2014

Linex, Prof Jay kuwasindikiza Kalapina, Q.Chilla Maisha Club

Kalapina
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Linex, Mapacha na Q Chillah ni baadhi ya watakaoshiriki kumsindikiza mkali wa Hip Hop nchini, Karama Masoud 'Kalapina' katika onyesho lake maalum.
Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika April 27 Maisha Club, kwa lengo la kuwaenzi wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wa kuisimamisha miondoko ya Hip Hop nchini.
Akizungumza na MICHARAZO, Kalapina alisema katika onyesho hilo ataimba 'live' wimbo wake mpya wa 'Hip Hop is Alive' alioimba na Q Chillah na kusindikizwa na mastaa kibao wa hip hop nchini.
Kalapina aliwataja baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Prof Jay, Kimbunga, Linex, Mapacha, Q Chilla mwenyewe na Masharikanz.
"Yaani itakuwa burudani ya kipekee kwa mashabiki wa Hip Hop na muziki wa kizazi kipya kwa ujumla kwa namna onyesho hilo maalum litakavyokuwa wakishuhudia Hip Hop is Alive ukiimbwa live," alisema.
Kalapina alisema katika onyesho hilo watapiga pia nyimbo zake zote pamoja na Kikosi cha Mizinga ambazo zilisaidia kuamsha harakati za kijamii kupitia miondoko hiyo ya hip hop nchini.

No comments:

Post a Comment