Chelsea ambayo ilimpoteza kipa wake nyota Petr Cech dakika ya 17 baada ya kuumia na baadaye nahodha wake, John Terry pia kwa majeraha, kwa kutoka suluhu hiyo kwenye uwanja wa Vincente Calderon, itahitaji ushindi wowote nyumbani dhidi ya Atletico.
Katika mfululizo wa ligi hiyo usiku huu timu za Real Madrid na mabaingwa watetezi Bayern Munich zitapepetana leo katika mchezo mwingine wa nusu fainali pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, mjini Madrid nchini Hispania.
Pambano hilo linarejesha kumbukumbu ya mechi ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa ya mwaka 2012 ambapo Bayern iliiondosha Madrid kwa mikwaju ya penati na kwenda kufa mikononi mwa Chelsea kwenye mchezo wa fainali.
No comments:
Post a Comment