STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 23, 2014

Burundi kutua nchini kesho kuifuata Stars

Burundi
TIMU ya Taifa ya Burundi 'Intamba Murugamba' inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Intamba Mu Rugamba itakuwa na msafara wa watu 28 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, na itafikia hoteli ya Accomondia. Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 jioni.
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000. Mechi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar

No comments:

Post a Comment