STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 24, 2015

Mkwasa aanza mambo Stars amrudisha Barthez

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhis1ruGzLmA1ni2IyaqnEsKPAAEcU8JO7z8W9li0En3Om_Boh3slIOKzhOTagB1Zu0FOQX-o3UpDYsxHBOmjwTFUuzSFtBgGlYmjZwAXkl0M_f-9MAmTsfs2ZcGHTmYwU-tCrQRuZ8DReg/s1600/Kocha+Mkwasa+%2528kushoto%2529+na+msaidizi+wake+Hemed+Morocco+wakiongea+na+waandishi+wa+habari.jpgKOCHA Mkuu Mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ameanza mambo yake baada ya kutangaza kikosi cha wachezaji 26 akimjumuisha kipa wa Yanga Ally Mustafa 'Barthez'.
Mkwasa alitangaza kikosi hicho kilichowajumuisha pia mshambuliaji wa JKT Ruvu Samuel Kamuntu, huku pia akitangaza jopo lake la Benchi la Ufundi atakalosimamia akisaidiana na Hemed Morocco.
Wachezaji walioitwa kwa ajili ya pambano la marudiano la kuwania kucheza fainali za Chan 2016 dhidi ya Uganda The Cranes ni; Makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).
Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).
Mawinga: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano “Messi” (Simba).
Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).
Wachezaji Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoingia kambini kesho.
Katika hatua nyingine Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahmed Mgoyi.
Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars

No comments:

Post a Comment