STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 26, 2015

Kazi imeanza, makocha Simba watua

Alianza huyu wa Kenya kwanza
Mwishowe wakakutana wote kwa pamoja
KLABU ya Simba imeonyesha haina utani baada ya makocha wake wapya Dylan Kerr kutoka Uingereza na Abdul Salim kutoka Kenya atakayewanoa makipa kutua nchini mchana huu wakitokea makwao.
Makocha hao wamelamba shavu la kuinoa Simba baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Goran Kopunovic kushindwa kuelewana na uongozi wa Rais Evans Aveva.
Kocha wa kwanza kutua nchini alikuwa Mkenya aliyewahi kuzinoa timu mbalimbali ikiwamo Gor Mahia na AFC Leopard ambaye alitua majira ya saa nane mchana kabla ya Kerry kutua saa 10 kwa Ndege ya Shirika la Emirates.
Makocha hao wametua tayari kuanza yao katika klabu hiyo ambayo kwa miaka mitatu sasa haijaonja taji la Ligi Kuu, huku ikiwa imebadilisha makocha wasiopungua watano tangu walipotwaa taji la mwisho msimu wa 2011-2012 ikiwa chini ya Cirkovic Milovan aliyefurshwa baadaye.
Kikosi cha wachezaji wa Simba kwa sasa wanajifua kwenye Gym ya Chang'ombe kabla ya kuanza rasmi mazoezi yao Julai Mosi ambapo Rais Aveva alidokeza kuwa itakuwa visiwani Zanzibar kwa muda wa majuma sita.
Hata hivyo Simba itaanza kambi hiyo bila baadhi ya nyota wake kadhaa wakiwamo wale waliopo katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa kuifuata Uganda the Cranes katika pambano la marudiano la kuwania fainali za CHAN-2016 zitakazofanyika Rwanda.
Wengine ambao hawatakuwapo ni Jonas Mkude aliyetimkia Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Afrika Kusini, huku Okwi akiwa kwao kwa ajili ya Fungate ya Arusi yao anayofunga kesho kwao Uganda na Raphael Kwireza akiwa amepewa mapumziko ya mwezi mmoja kusikilia majereha yake yanayomtibulia kukipiga Msimbazi licha ya kuwa na mkataba wa miaka miwili unaomalizika mwakani.

No comments:

Post a Comment