STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 26, 2015

TFF yavichimba mkwara vyama vya soka mikoani

KUFUATIA pendekezo la sekretariet ya TFF ambalo baadae lilipitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF kila mkoa unatakiwa kuwa na kituo chake cha kulea na kukuza vipaji vya mpira wa vijana umri kuanzia miaka 8-17.

Kwa mikoa ambayo tayari ina kituo ambacho inakiendesha yenyewe TFF inaonba ipatiwe taarifa hiyo ikiwa ni pamoja na kufahamishwa jina la kituo, jina la mwalimu na sifa zake na utaratibu wa mafunzo.

Kwa mikoa ambayo haina kituo TFF inagiza mikoa hiyo kuingia ubia na kituo kimoja ambacho tayari kina program ya kukuza na kuendeleza vipaji ili kijulikane kuwa ni kituo maalum cha mkoa husika.

Katika hilo TFF inaagiza kamati ya utendaji ya mkoa husika iandae muhtasari wa kikao cha utendaji cha chama cha mkoa wa kupitisha maamuzi hayo, MoU (makubaliano rasmi) yasainiwe kati ya chama cha mkoa na kituo husika na hati hiyo nakala yake iletwe TFF.

MoU hiyo ionyeshe majukumu ya chama cha mpira cha mkoa kama kutoa vifaa, kutoa mwalimu, usimamizi nk na pia kuonyesha majukumu ya mwenye kituo kama kutoa uwanja,ulinzi nk. MoU itaonyesha pia nani atafaidika na vipaji vitakavyoibuliwa kati ya mzazi,kituo na chama cha mkoa.

TFF itaandaa MoU ya mfano kwa ajili ya vyama vyote vya mikoa na ingependa kufikia tarehe 31/Desemba/2015 kila mkoa uwe umetekeleza jambo hilo
.

No comments:

Post a Comment