STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 26, 2015

Jennifer Mgendi kufanya tamasha kubwa Dar Jumapili

http://1.bp.blogspot.com/-5DRz9Os0TvI/VL4GP0fwaMI/AAAAAAAAOXk/_Pj7wlU7Ryo/s1600/MGENDI.JPG
Jennifer Mgendi
MUIMBAJI nyota wa muziki wa Injili ambaye pia ni muigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini, Jennifer Mgendi anajiandaa kuifanya tamasha kubwa kwa ajili ya Kumshukuru Mungu kwa kuweza kudumu kwenye fani hizo kwa miaka 20 sasa.
Jennifer alidokeza kuwa Tamasha hilo lililopewa jina la 'Tamasha la Miaka 20 ya Shukrani litafanyika kwenye Kanisa la DCT lililopo Tabata Shule karibu na Kituo cha Polisi Tabata siku ya Jumapili Juni 28 na kusindikizwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili nchini.
"Natarajia kufanya tamasha la Shukran ya Miaka 2o, litakalofanyika Juni 28 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa TIG, Dk Barnabas Mtokambali na waimbaji mbalimbali watanisindikiza akiwamo Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Cosmas Chidumule, Ency Mwalukasa, Mchungaji Charles Jangalason na wengineo," alisema Jennifer.
Jennifer alisema ana haki ya kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kumpa kipaji na kumwezesha kudumu katika huduma ya uimbaji kwa miaka hiyo yote 20.
Muimbaji huyo kwa sasa anatamba na albamu nane za muziki wa Injili tangu alipojitosa kwenye fani hiyo mwaka 1995 na katika tamasha hilo ataizundua video ya albamu yake inayotamba sasa ya 'WEMA NI AKIBA'.
Mbali na kwenye muziki, Jennifer pia anatamba kwenye filamu akiwa anakimbiza kwa sasa na kazi zake kadhaa ukiwamo 'Teke la Mama', 'Chai Moto', 'Pigo la Faraja', 'Mama Mkwe' na nyinginezo ambazo zimemfanya kuwa matawi ya juu licha ya kwamba hana makeke kama wasanii wengine.

No comments:

Post a Comment