STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, March 6, 2015

Dokii afichua kilichomkimbiza Yanga kwenda Azam

Dokii
MUIGIZAJI nyota aliye pia muimbaji wa muziki, Ummy Wenceslaus 'Dokii' ambaye alikuwa mmoja wa mashabiki wakubwa wa Yanga amefichua siri ya kutangaza kuitema timu hiyo na kujiunga kuishangilia Azam FC.
Akizungumza na MICHARAZO katika mahojiano maalum kwa njia ya simu, Dokii alisema ameamua kuitosa Yanga ambayo keshokutwa itashuka dimbani kuvaana na Simba kutokana na kuvutiwa na uwezo wa wachezaji pamoja na viongozi wa klabu hiyo ya Azam.
"Kilichonifanya kuitosa Yanga na kuhamia Azam ni ubora wa wachezaji na uongozi wa jumla," alisema.
Alipoulizwa ataendelea kuishabikia Azam hata kama imeng'oka michuano ya kimataifa alipoibukia kwa mara ya kwanza wakati timu hiyo ikiumana na El Merreikh na kushinda 2-0, Dokii alisema Azam milele kwake kwani ni moja ya timu yenye muono wa mbali wa kimaendeleo.
"Vyovyote iwavyo mimi na Azam, nitaishangilia na kuipa sapoti kokote ilipo hata kama hatuendelei michuano ya kimataifa," alisema Dokii.
Dokii aliyekuwa miongoni mwa wasanii wanaoizimikia Yanga alionekana 'bize' uwanja wa Azam akishangilia timu hiyo akijipamba 'ki-Azam' tofauti na alivyozoeleka na hata kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi alikuwa akiishangilia timu yake ya Yanga iliyotoka robo fainali.

No comments:

Post a Comment