STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 8, 2013

Dogo Aslay bado mdogo kwa Linnah


MSANII anayezidi kuja juu nchini, Aslay Is'haka 'Dogo Aslay' anaandaa video ya wimbo wake mpya uitwao 'Bado Mdogo' aliomshirikiana na mkali wa THT, Linnah.
Akizungumza na MICHARAZO, Meneja wa Aslay, Said Fella, alisema wimbo huo ulioanza kutamba kwenye vituo mbalimbali vya redio utarekodiwa video yake kuanzia Julai 10 katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam.
Fella alisema walikuwa waanze kazi hiyo wiki hii, lakini muingiliano na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama imewafanya wasongeze mbele hadi wiki hii.
"Kutoka kwa Mkubwa na Wanawe, tumeachia wimbo mpya wa Aslay uitwayo 'Bado Mdogo' alioimba na Linnah wa THT na video yake ilikuwa irekodiwe wiki hii, lakini tumesogeza mbele hadi Julai 10 kupisha ziara ya Rais wa Marekani," alisema Fella.
Wimbo huo wa 'Bado Mdogo' utakaorekodia video yake ya kampuni ya Visual Lab ya Adam Juma, ni kibao cha sita kwa Aslay baada ya kutoka na 'Niwe Nawe', 'Nakusemea', 'Umbeambea', 'Wahenga' na 'Nitachezaje'.
Alisema bado kuna kazi nyingine za msanii huyo aliyeibuliwa kupitia Kituo cha Mkubwa na Wanawe, ambazo zitakuwa zikiachiwa moja baada ya nyingine.

No comments:

Post a Comment