[BARAKAEL MASAKI - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WATU wanaosadikiwa kuwa majambazi wamemuua kwa kumkataka kwa mapanga Mlinzi binafsi anayefahamika kwa majija ya Oden Mkumbwa (60) akiwa katika lindo lake eneo la Mbata, jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi mkoani humo, Mlinzi huyo alivamiwa na watu wasiofahamika akiwa katika lindo lake duka la dawa muhimu (Phamacy) na kumuua kabla ya kuvunja duka hilo na kuimba dawa za aina mbalimbali pamoja na fedha taslim Sh. 600,000.
Polisi wamesema mlinzi huyo ni mwenyeji wa eneo la Nonde na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya wakati jeshi linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo ili kuwanasa wahusika.
Chini ndiyo taarifa rasmi ya jeshi hilo na matukio mawili ya ajali barabarani zilizosababisha vifo vya watu watatu katika maeneo la Ileje na wilayani Rungwe.
WILAYA YA MBEYA MJINI - MAUAJI
MNAMO
TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA USIKU HUKO MTAA WA MBATA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ODEN
S/O MKUMBWA, MIAKA 60, MNDALI, MLINZI BINAFSI MKAZI WA NONDE ALIUAWA KWA
KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALI MBALI ZA MWILI WAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA
AKIWA KAZINI KATIKA LINDO AMBALO NI DUKA LA MADAWA MUHUMU [PHAMACY] LILILOPO
ENEO HILO. MBINU ILIYOTUMIKA NI
WATUHUMIWA KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA KATIKA LINDO NA KUMUUA KISHA KUVUNJA DUKA HILO LA DAWA
MUHIMU NA KUIBA DAWA ZA AINA
MBALIMBALI PAMOJA NA FEDHA TASLIMU TSHS 600,000/=. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA
KIFO.
MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA
SAA 15:30HRS HUKO ILIMA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA.
GARI T.654 BPX AINA YA TOYOTA
COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA IMANI S/O MWAKILEMA,MIAKA 34,KYUSA, MKAZI WA
KYELA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MAGE D/O NSUKEMO,MIAKA 59,KYUSA,MKULIMA
,MKAZI WA ILIMA NA KUMSABABISHIA KIFO CHAKE MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU KWA AJILI YA MATIBABU. CHANZO NI MWENDO KASI. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA
VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA ILEJE - AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA
VIFO.
MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA
SAA 20:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBEBE WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. GARI
NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI T. 863 BXC AINA YA SANYA AITWAE OBADIA S/O
MWAKIPESILE,MIAKA 36,KYUSA,MKAZI WA MBEBE PAMOJA NA ABIRIA WAKE FRED S/O
FUMBIKA,MIAKA 23,MNDALI,FUNDI UJENZI MKAZI WA ISANGA MBEYA NA KUSABABISHA VIFO
VYAO PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI.
MIILI YA MAREHEMU
IMEHIFADHIWA HOSPITALINI YA WILAYA YA ILEJE. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA
BAADA YA TUKIO .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI BARAKAEL MASAKI. ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed By,
[BARAKAEL MASAKI - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
No comments:
Post a Comment