STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 8, 2013

Kajala ana Heart Attack

Kajala Masanja katika pozi

MSANII Winfrida Masanja maarufu kama Kajala Masanja, amerejea kwenye fani baada ya msukosuko wa kunusurika kwenda jela kwa kuibuka na filamu yake binafsi iitwayo 'Heart Attack' aliyoigiza kama msichana wa kijijini anayefanyiwa unyanyasaji wa kutisha.
Filamu hiyo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika kwake Kajala ameigiza kwa kushirikiana na wasanii wakongwe na wenye majina majina nchini.
Baadhi ya wasanii hao walioigiza na mwanadada huyo aliyewahi kutamba na filamu kadhaa zikiwamo 'Devil's Kingdom, Kijiji Chatambua Haki, Dhuluma na nyingine ni pamoja na Mohammed Fungafunga 'Jengua', Fatuma Makongoro 'Bi Mwenda' na Lumole Matovolwa 'Biggie'.
Katika filamu hiyo Kajala anacheza kama msichana anayelelewa na Jengua na Bi Mwenda ambao ni mke na mume ambao ni wazazi walezi kwa Kajala, lakini wenye roho mbaya na wakali kupindukia ambao wanampa wakati mgumu yeye na ndugu zake.
Hiyo ni moja ya kazi mpya tangu Kajala anusurike kwenda jela baada ya kukutwa na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na mumewe kabla ya Wema Sepetu kumlipia faini ya Sh Milioni 13 na kuokoka na kifungo kama ilivyomkuta mumewe.

No comments:

Post a Comment