STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 8, 2013

Wachumba wanaswa na dawa za kulevya uwanja wa JK

Kamanda Nzowa

WATU wawili  mtu na mchumba wake wamekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakiwa na kilo mbili za dawa za kulevya aina ya Heroin zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 90.
Kamanda wa Polisi Kikosi Maalumu cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alisema jana kuwa watu hao walikamatwa juzi saa 8.00 mchana katika uwanja huo, baada ya kushtukiwa na askari.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ramadhan Shabani (37) na mchumba wake Pendo Msacky (32), wote wakazi wa Mikocheni A na walikuwa wakienda Bangkok.
Kamanda Nzowa alisema Shabani alikutwa na hati ya kusafiria yenye namba AB 427507, huku mchumba wake akiwa na hati ya kusafiria yenye namba AB 211609.
Alisema kila mmoja alikutwa akiwa ameficha dawa kilo moja kwenye begi lake, na walikuwa wasafiri na ndege ya Shirika la Ethiopia (Ethiopian Airlines).

No comments:

Post a Comment