STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 1, 2014

Mkurugenzi Zugo Sports ahimiza wanawake kujifunza Martial Arts

Zuwena Idd Kipingu akionyesha umahiri kwa kunyanyua chuma katika gym yake
WANAWAKE na wasichana wamehimiza kujenga utamaduni ya kupenda kujifunza na kucheza michezo ya mapigano kwa lengo la kuwasaidia kuwaepusha na matukio la kudhalilishwa mitaani.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Klabu ya Michezo ya Zugo, Zuwena Idd Kipingu, alipozungumza na blogu hii na kudai ili kuepukana na kubakwa au kuporwa na unyanyasaji mwingine wasichana na wanawake wanapaswa kujifunza na kucheza michezo ya mapigano (Martial Arts).
Zuwena alisema michezo hiyo mbali na kuwaweka kuwa fiti pia itawasaidia kwa ulinzi wao binafsi pale wanapovamiwa au kukumbana na wahalifu mahali popote.
"Wanawake na wasichana wamekuwa wakifanyiwa uonevu na baadhi ya wanajamii kwa kuwaona ni wanyonge na legelege ni fursa yao kujifunza michezo kama ya karate, Judo, Kung-fu au ngumi ili kujiweka fiti na kukomesha unyanyasaji dhidi yao," alisema.
Mkurugenzi huyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) alisema klabu yake ipo tayari kuwapa mafunzo wanawake wanaohitaji kufanya hivyo.
"Klabu yangu ya Zugo Sports, inafundisha michezo mbalimbali, lakini wengi wao ni wanaume, nilidhani ni wakati wanawake na wasichana wakachangamka ili kujisaidia kwa mambo mengi."
Alisema mbali na kupata ulinzi binafsi katika matukio madogo madogo, lakini pia michezo itawafanya wawe na afya njema pamoja na kujitengenezea mazingira mazuri ya ajira.
Mwanadada huyo mwenye mkanda mweusi katika mchezo wa Taekwondo na aliyewahi kung'ara kwenye michezo ya kunyanyua vitu vizito na ngumi, alisema wanawake wasijiweke nyuma.
"Wasijiweke nyuma au kutishwa na madai kwamba ukicheza michezo kama hiyo hataweza kuzaa, huo ni uongo mimi nimeanza michezo hii mwaka 1980 na nina watoto saba kwa sasa," alisema.
Aliongeza kuwa, michezo ni afya, hivyo ni wajibu hata kwa wazazi kuwazoesha watoto wao kuicheza ili kuiweka miili yao salama na kuepukana na maradhi madogo madogo.

No comments:

Post a Comment