STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 26, 2014

TPBO-Limited yaitisha mkutano wa wadau wa ngumi jijini Dar


WADAU wa ngumi za kulipwa nchini wanatarajia kukutana katika mkutano wa pamoja ulioitishwa na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO-Limited) ili kujadili mustakabali wa mchezo huo kwa mwaka 2014.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Oganaizesheni hiyo, Ibrahim Kamwe mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Vijana Social, Kinondoni na utahudhuriwa na wadau wote wa ngumi hizo nchini.
Miongoni mwa wadau ambao ndiyo walengwa wakuu wa mkutano huo uliofadhiliwa na Kitwe Traders ni;  makocha, mabondia, mapromota, waamuzi na watu wote ambao wamekuwa bega kwa bega na mchezo huo.
Kamwe alisema  lengo kuu la mkutano huo ni kujadili namna ya kuupelekea mbele mchezo huo ambao pamoja na kutokuwa na wadhamini, lakini dniyo ambao umekuwa ukiiletea sifa Tanzania kwa mabondia wake kunyakua mataji ya kimataifa.
Alisema wamewaalika pia viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wadau wengine wakiwamo viongozi wa mashirikisho ya ngumi hizo nchini kama akina Emmanuel Mlundwa wa PST, Onesmo Ngowi wa TPBC.
"Mkutano huo utahudhuriwa na wadau wengine wakiwemo makondia wastaafu kama akina Matumla, Habib Kinyogoli, Names Kavishe, Zuwena Kibena na wadau ambao wamekuwa wakiusaidi kusonga mbele ili tujadili na kupanga mikakati ya mwaka 2014," alisema Kamwe.
Alitoa wito kwa yeyote ambao anajitambua kuwa ni mdau wa ngumi za kulipwa nchini wakipata taarifa yake wasisite kujitokeza kwenye ukumbi wa mkutano huo kwa lengo la kufanikisha yale wanayotaka yawe.

No comments:

Post a Comment