STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 9, 2014

Francis Cheka kuzipiga na Pascal Ndomba

Francis Cheka
Pascal Ndomba
BINGWA wa zamani wa Dunia wa WBF, Francis Cheka anatarajiwa kupanda ulingoni siku ya Novemba Mosi kupigana na bondia Pascal Ndomba katika pambano lisilo la ubingwa litakalofanyika mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) Chaurembo Palasa, pambano hilo la uzito wa juu litachezwa kwenye uwanja wa Sabasaba mjini humo.
Palasa alisema TPBC imetoa baraka zote kwa pambano hilo litakalokuwa la raundi 10.
Rais huyo alisema mchezo huo na mingine ya utangulizi siku hiyo imeandaliwa na kampuni ya Cheka Promotion na mabondia watakawasindikiza wanatarajiwa kutangazwa baadaye.
Hilo litakuwa ni pambano la kwanza kwa mabondia hao kukutana na pia la kwanza kwa Cheka tangu bondia huyo alipopanda ulingoni mara ya mwisho  Aprili 19 mwaka huu alipopigana na bondia toka Iran Sajad Mehrabi  na kutoka naye sare kwenye ukumbi wa PTA.
Cheka ndiye bondia asiyepigika nchini kwa sasa akiwa amewatandika karibuni wapinzani wake wote tangu mwaka 2008 hajapigwa, ingawa anapotoka nje ya nchi amekuwa 'urojo'.

No comments:

Post a Comment