STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 9, 2014

Didier Zakora atundika daluga kuichezea Tembo wa Ivory Coast

http://images.supersport.com/2014/5/Didier-Zokora-100615-Gestures-R300.jpg 
http://futboler.tv/wp-content/uploads/2014/05/fft99_mf1310873.jpegKIUNGO nyota wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Zokora ametangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya kuitumikia timu ya taifa kwa zaidi ya miaka 10. Maestro kama anavyofahamika kwa mashabiki wa soka nchini mwake, alisema anadhani ni muda muafaka kuwapisha wengine kuitumikia timu hiyo.
"Baada ya miaka 15 ya kucheza soka ya kiwango cha juu, nafikiri ni wakati wa mimi kufikia tamati ya soka soka ya kimataifa" amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 katika mashindano maalum yaliyoandaliwa kwa heshima yake mjini Abidjan kitongoji cha Williamsville."Ni wakati wa kutoa nafasi kwa vijana wadogo. Katika mechi na Sierra Leone, nimeona wachezaji wadogo ambao wanaweza kuchukua nafasi," aliongeza.
Zokora alianza kuichezea timu hiyo tangu mwaka 2000 na amekuwa na rekodi ya kucheza mechi 121.
Amecheza fainali tano za Kombe la Mataifa ya Afrika mfululizo 2006, 2008, 2010, 2012 na 2013, mbali na  Kombe la Dunia mara tatu mfululizo 2006, 2010 na 2014.
Kiungo huyo mkabaji, kwa sasa anachezea klabu ya Akhisar Belediyespor ya Uturuki, baada ya kuchezea klabu nyingine za Racing Genk ya Ubelgiji, Saint-Etienne ya Ufaransa, Tottenham Hotspur ya England, Sevilla ya Hispania na Trabzonspor ya Uturuki pia.
Ni matunda ya akademi ya ASEC Mimosas ya mwaka 1998 ambao walishinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga Dynamos ya Zimbabwe kwenye fainali, michuano ambayo pia Yanga SC ilishiriki.
Zokora ambaye majina yake kamili ni
Déguy Alain Didier Zokora alizaliwa Desemba 14, 1980) ni gwiji mwingine wa Ivory Coast kustaafu kwa sasa baada ya Nahodha wa zamani, Didier Drogba anayechezea Chelsea.

No comments:

Post a Comment