STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 9, 2014

Simanzi! Paroko wa RC afa ghafla

http://sw.radiovaticana.va/storico/2013/03/files/imm/1_0_669336.JPG 
BAADHI ya waamini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Fatma mjini Geita, wameshitushwa na taarifa za kifo cha Paroko wa Parokia ya Geita, Padri Henry Kimisha aliyefariki dunia ghafla jana asubuhi.
Akitoa taarifa za kifo hicho, Msaidizi wa Askofu Jimbo Katoliki la Geita, Padri Nikodema Duba, alisema saa mbili asubuhi padre huyo aliugua ghafla na kulazimika kwenda hospitali ya wilaya ya Geita huku wakifanya maandalizi ya kumpeleka hospitali ya misheni Sengerema, lakini ghafla akafariki dunia.
Msaidizi huyo alisema Paroko Kimisha alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu, ugonjwa uliokatisha maisha yake ghafla huku akibainisha kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Bugando.
Padri Kimisha aliyezaliwa Juni 8, 1967 katika Kijiji cha Katunguru wilayani Sengerema, Mwanza na kupata daraja la upadrisho Julai 25, 1996 kwenye Parokia ya Nyantakubwa wilayani humo, maziko yake yatafanyika Ijumaa kwenye makaburi ya kanisa hilo.
Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment