Wachezaji wa Everton wakishangilia ushindi wao dhidi ya Sunderland |
Everton ikiw augenini iliichapa Sunderland kwa bao 1-0 na kuzidi kuiweka pabaya wapinzani wao katika janga la kuepuka kushuka daraja na kuwafanya wafikise jumla a pointi 66, mbili zaidi ya Arsenal hawakucheza ligi kwa vile walikuwa wakikabiliwa na mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la FA.
Bao la kujifunga la West Brown wa Sunderland lilitosha kuwapa wageni ushindi huo muhimu na kuwafanya kuanza kupata uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani kama mambo yataenda yalivyo na hasa Arsenal kama itaendelea kuzembea kwenye mechi zake ambapo zimeifanya itoke kileleni mwa msimamo hadi kushika nafasi ya tano sasa.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Spurs ikiwa ugenini ililazimisha sare ya mabao 3-3 dhidi ya West Brom katika pambano ambalo lilionekana wazi kama Tottenham wanakufa ugenini kwa mara nyingine kwani hadi mapumziko walikuwa nyuma kwa mabao 3-1, bao lao likiwa ni la kujifunga kwa wenyeji.
Vydra aliwashtukiza wageni wa dakika ya kwanza kwa kuandika bao la kuongoza kabla ya Brunt kuongeza la pili dakika tatu baadae na Sessègnon kufunga bao la tatu dakika ya 31 na Olsson aliwapa wageni takrima kwa kujifunga dakika ya 34.
Hata hivyo kipindi cha pili kucheza kwao kwa kujihami kuliwaponza wenyeji baada ya wageni Spurs kuingia kpindi hicho wakiwa kivingine kwa kufanya mashambuilizi mfululizo na kufanikiwa kurejesha bao moja hadi jingine.
Harry Kane aliifungia Spurs bao la pili dakika ya 70 akimalizia krosi ya Aaron Lennon na katika dakika nne kati ya sita za nyongeza Christian Eriksen aliisawazishia Spurs bao na kuambulia pointi moja na kuwafanya wafikishe pointi 60 na kusalia kwenye nafasi ya sita juu ya Manchester United wenye pointi 57.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Crystal Palace wakiwa nyumbani walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi Aston Villa, huku
Fulham ikitaka pia nyumbani kwa ushindi kama huo wa bao 1-0 dhidi ya Norwich City na Cardiff City wakatamba ugenini mwa Southampton kwa kuilaza 1-0 na Newcastle United ikazabuliwa bao 1-0 ugenini na Stoke City.
No comments:
Post a Comment