STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 13, 2014

Prisons yaishusha rasmi Rhino, Coastal yafa tena

Prisons iliyoishusha daraja Rhino
PRISONS-Mbeya ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani imeifumua Rhino Rangers na kuishusha rasmi Ligi Daraja la Kwanza baada ya kuilaza mabao 4-3 , huku JKT Ruvu ikijiokoa katika janga hilo kwa kuizabua Coastal Unio kwenye uwanja wa Mkwakwani kwa bao 1-0.
Katika pambano la uwanja wa Sokoine kulikuwa na funga nikufunge, huku wenyeji wakitangulia mabao 2-1 hadi wakati wa mapumziko, hata hivyo kipindi cha pili walirejesha bao na kuongezwa na lal tatu kabla ya kucharuka na rufunga mabao mengine mawili yaliyohitimisha safari ya Rhino kwenye Ligi Kuu baada ya kuipanda msimu huu.
Nayo Coastal Union imeendelea kuwa 'jamvi la wageni' baada ya kunyukwa bao 1-0 na JKT Ruvu na kuwafanya mafande hao kujihakikishia kusalia Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao kwa kufikisha pointi 31.
Bao lililowapa ushindi maafande hao wanaonolewa na kocha Fred Felix Minziro lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Gido Chawala na kuifanya Coastal ipokeaa kipigo cha tatu mfululizo tangu walipoilaza Simba jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo ilifungwa na Mtibwa Sugar mabao 3-1 kabla ya Mgambo kuwasulubu kwa mabao 2-0 na kufuatiwa na kipigo hicho cha JKT.

No comments:

Post a Comment