STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 18, 2014

STAND UNITED YAIKATIA RUFANI KANEMBWA JKT

Vurugu  za mechi ya awali baina ya Stand Utd na Kanembwa JKT

TIMU ya soka ya Stand United ya Shinyanga imekata rufani Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikipinga Kanembwa JKT ya Kigoma kuchezesha wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo kwenye mechi ya kiporo iliyozikutanisha timu hizo.
Mechi hiyo namba 22 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilichezwa juzi (Februari 16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Kanembwa JKT iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Katika rufani yake, Stand United inadai kwenye mechi hiyo Kanembwa JKT ilichezesha wachezaji wanane waliosajiliwa katika dirisha kidogo kinyume na maelekezo kutoka TFF kwa timu hizo kuwa wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo hawawezi kucheza mechi hiyo.
Wachezaji wanaodaiwa kusajiliwa dirisha dogo na kucheza mechi hiyo ni Hamidu Juma, Ibrahim Shaban Issa, Joseph Mlary, Lucas Charles Karanga, Raji Ismail, Salvatory Kulia Raphael, Seif Ibrahim Zaid na Yonathan David Sabugowiga.
Dirisha dogo lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka jana, hivyo Stand United katika rufani yake inaombwa ipewe pointi tatu na mabao matatu kwa Kanembwa JKT kuchezesha wachezaji wasiostahili.
Awali mechi hiyo ilichezwa Novemba 2 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, na kuvunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya Kanembwa JKT kugomea pigo la penalti dhidi yao.

No comments:

Post a Comment