STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 16, 2013

Fabregas azikata maini Arsenal, Man United

2013 cesc fabregas barcelona
Cesc Fabregas

SIKU moja tu baada ya klabu ya Manchester United kutangaza kuongeza dau ili kumnasa nahodha wa zamani wa mahasimu wao Arsenal, Cesc Fabregas, kiungo huyo ameikata maini timu hiyo.
Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Hispania anayeichezea Barcelona alikuwa chaguo la kwanza la David Moyes baada ya kumkosa Thiago Alcantara, pia alikuwa akiwindwa na klabu yake ya zamani. Hata hivyo  kocha wa Barcelona, Tito Vilanova amefichua kuwa,  aliongea na kiungo huyo na kumwambia kuwa kwamba anahitaji kuendelea kubaki Camp Nou.
Jana iliripotiwa kwamba United walituma ofa ya kwanza ya kiasi cha £25.9 million  kwa ajili ya kumsajili Fabregas, ambaye amefeli kupata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu aliporudi akitokea Arsenal.
Lakini akiongea na waandishi wa habari leo mchana, Vilanova amesema wazi kwamba Fabregas bado anataka kubaki kwenye klabu yake hiyo ya utotoni, na hana mawazo ya kuondoka.
 "Ninafahamu kwamba tumepokea ofa kadhaa kutoka kwa vilabu tofauti. Niliongea na Cesc na ameniambia kwamba anataka kubaki.
"Cesc hana mawazo ya kuondoka kwenda klabu nyingine. Anajua ushindani ni mkubwa hapa na ana ndoto za kuendelea kuwa hapa na kufanikiwa.


No comments:

Post a Comment