STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 2, 2013

Vital'O ya Burundi yairithi Yanga taji la Kagame 2013

Mabingwa wapya wa Kagame Cup, Vital'o wakishangilia taji lao

TIMU ya soka ya Vital'o ya Burundi jana ilifanikiwa kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Kagame wakiwarithi Yanga iliyokuwa bingwa mtetezi na kutokwenda kwenye michuano hiyo, baada ya kuilaza majirani zao APR ya Rwanda kwa mabao 2-0 katika mechi ya fainali.
Hilo ni taji la kwanza kwa timu hiyo katika historia ya michuano hiyo na ilifanikiwa kupata ushindi huo katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa El Fasher, Darfur nchini Sudan na kumaliza michuano hiyo bila kupoteza mechi yoyote.
Mabao ya washindi hao ambao waliing'oa timu nyingine ya Rwanda Rayon katika mechi ya nusu fainali yalitumbukizwa wavuni katika kipindi cha pili na Tambwe Amisi ambaye pia aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga mabao 6 kabla ya dakika tatu baadaye Christian Mbirizi kuongeza la pili na kuzima ndoto za wapinzani wao waliokuwa wakiwania taji la nne.
Wawakilishi wa Tanzania Simba, Falcon ya Zanzibar na waliokuwa watetezi wa taji hilo, Yanga hawakwenda katika michuano hiyo kwa hofu ya kutokuwepo amani na kufanya michuano hiyo kukosa msisimko japo yalichezwa na kumalizika salama bila tukio lolote kama ilivyokuwa ikitangazwa na wanasiasa wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment