STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 3, 2014

Madee kuweka shida zake videoni

http://4.bp.blogspot.com/_43Ui7xqwc_E/TIeMqUIJjVI/AAAAAAAAAA0/xFDGRaAVXwI/s1600/Mtu+mzima+Madee.jpg
Madee katika pozi
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Hamad Ally 'Madee' a.k.a Rais wa Manzese, anajianda kuanza kurekodi video ya wimbo wake mpya unaoendelea kutamba katika vituo vya redio uitwao Ni Sheeda'.
Akizungumza na MICHARAZO, Madee alisema ndani ya wiki mbili zijazo video ya wimbo huo itakuwa hewani kwani ameanza maandalizi ya kuirekodi.
Madee alisema video hiyo itarekodiwa na kampuni ya Next Level Production chini ya mtaalam Adam Juma na itafanyiwa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam.,
"Nipo katika maandalizi ya kurekodi video ya wimbo wangu mpya wa 'Ni Sheeda' (Ni Shida) kazi hiyo itafanywa na Adam Juma na huenda ikakamilika ndani ya wiki mbili kabla ya kuiachia hewani," alisema.
Madee alisema anaharakisha kutoa video hiyo kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa muziki ambao wanataka kuona uhalisia wa wimbo huo ambao umekuwa gumzo kwa sasa nchini.
"Mashabiki wamekuwa wakiulizia mno juu ya video yake ndiyo maana nataka kuitoa mapema kabla ya kufanya mambo mengine," alisema Madee.
Mkali huyo anayeliongoza kundi la Tip Top Connection, kabla ya wimbo huo wa 'Ni Sheeda' Madee alitamba na nyimbo kama 'Pesa', 'Kazi yake Mola', 'Tema Mate', 'Pombe Yangu', Hip Hop Haiuzi na 'Yote Maisha'.

No comments:

Post a Comment