STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 3, 2014

Taifa Stars kufanya maajabu Maputo Leo

http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/05/DSC_457511.jpgLICHA ya Taifa Stars kuwa na pambano gumu leo mjini Maputo, Msumbiji itakaporudiana na wenyeji wao, Mambas baadhi ya nyota wa timu hiyo wametamba kufanya maajabu.
Stars ambayo imekuwa ikinyanyaswa na Mambas inahitaji ushindi wowote ili kupenya hatua ya makundi ya kuwania kucheza Fainali za AFCON-2015 zitakazochezwa Morocco.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita, Stars ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dakika za mwishoni na kujiweka katika wakati mgumu kwa mechi hiyo ya ugenini.
Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wametamba kabla ya kuelekea Maputo kwamba watafanya maajabu ambayo wengi hawayatarajii kwa kuing'oa Mamba kwao.
Nahodha wa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro', kipa Deo Munishi 'Dida' na John Bocco kwa nyakati tofauti walisema kuwa wana ari kubwa ya kulipigania taifa leo Maputo.
"Ni kweli mechi yetu itakuwa ngumu kwa vile tutakuwa ugenini, ila tumejipanga kuhakikisha tunaivusha Stars hatua ya makundi na Inshallah mtuombee," alisema Cannavaro.
Cannavaro alisema wachezaji wamezingatia maelekezo ya kocha Mart Nooij baada ya kufanya uzembe katika mechi iliyopita ambapo Stars walikuwa mbele kwa mabao 2-1 hadi dakika ya 87 kabla ya wageni Msumbiji klusawazisha.
Dida kwa upande wake alisema kila mchezaji wa Stars anajua wajibu wake kwa siku ya leo Jumapili mjini Maputo na amewaomba watanzania waungane nao kwa dua njema.
Msumbiji imekuwa na zali la kuikwamisha Stars kila inapokutana katika hatua kama hiyo ya kuwania kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mara ya kwanza waliwazuia kwenda fainali za Ghana za mwaka 2008 na mwaka jana ilirudia tena na kuwafanya mashabiki wa soka kuamini Stars leo ina kazi ngumu Maputo.
Kama Stars itapenya kwa Mambas, itaangukia katika kundi F ambalo litakuwa na timu za Zambia, Niger na Cape Verde ili kuanza kusaka tiketi ya kwenda Morocco mwakani.

No comments:

Post a Comment