STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 3, 2014

Hivi ndivyo mahafali ya kwanza ya Pre Primary Joyland yalivyofana

Mgeni Rasmi wa Mahafali hayo Bi Bushra Malik Regional Development Manager wa Edexcel akizungumza kwenye shughuli hiyo zilizofanyika jana Kigamboni, Dar es Salaam
Mmoja wa wahitimu wa kozi ya Kiingereza inayotolewa bure shuleni Joyland akipokea cheti chake toka kwa Bi Bushra Malik

Mmoja ya wanafunzi waliofanya vyema katika mitihani akipewa zawadi yake na mmoja wa wageni waalikwa wa hafla hizo
Mwanafuzi Ansilath Kwariko akilia kwa furaha wakati akijiandaa kupokea zawadi yake
Madogo kwa kuimba hawajambo
Wahitimu wa Pre Primary wakiongozwa na mwalimu wao kuingia eneo la tukio
Sisi tunajua kuimba
Mkurugenzi wa Joyland International School, Fredrick Otieno akisaini mkataba wa kurushwa kwa vipindi vya shule yake na kituo cha Channel Ten huku akishuhudiwa na mwakilishi wa Idara ya Masoko ya kituo hicho

Saini hapa.....Tutakurusha hewani mpaka basi! Mwakilishi wa Channel Ten akimuangalia Mkurugenzi wa Shule ya Kimataifa ya Joyland akisaini mkataba walioingia baina yao kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa kwenye hafla hiyo jana.
Wanafunzi wa Grade 5 wakitumbuiza

Siyo kuhitimu tu hata kuimba nasi tunajua
Mkurugenzi wa Joyland, Fredrick Otieno  akionyesha ufundi wa kucheza akichuana na wanafunzi wake

Yebhaa! Mnacheza hivi bhana!
Full Vipaji Joyland International School
Hongera kwa kumaliza kozi!
Msosi nao ulikuwapo kuwafariji wahitimu

Kadhalika vinjwaji navyo viliburudisha makoo ya watoto

Tupo makini na watoto wenu, tunawaangalia vya kutosha kuhakikisha wapo salama
Mkurugenzi wa Joyland International School, Fredrick Otieno akizungumza kwenye hafla hiyo
WAZAZI na walezi nchini wamehimizwa kuwapatia elimu watoto wao ili kuwajengea msingi imara wa maisha yao kwa kuwa, elimu ni hazina isiyoweza kuharibika au kuibwa na yeyote.
Aidha wazazi na walezi pia wamekumbushwa kujenga utamaduni wa kuwa na mahusiano mazuri baina yao na walimu wanaosoma watoto wao sambamba na kufuatilia nyendo za watoto wao ili kulinda wasiharibike.
Wito huo ulitolewa juzi na Mkurugenzi wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, Fredrick Otieno wakati akizungumza na wazazi na walezi waliohudhuria mahafali ya kwanza ya wahitimu wa Chekechea wa shule hiyo.
Otieno alisema elimu ndiyo msingi wa kila kitu kwa maisha ya binadamu, hivyo wazazi wajenge utamaduni wa kuwa wepesi kuwasomesha watoto wao ili kuwajengea msingi mzuri wa mustakabali wa maisha yao ya ukubwani.
Alisema wapo baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wepesi kuwanunulia watoto wao vitu vyenye thamani, lakini wanakuwa wagumu kuwalipia watoto ada au kuwapatia elimu bora bila kujua kama wanawaharibia maisha yao ya ukubwani ambayo hujengwa na elimu bora ya utotoni.
"Dunia ya sasa imebadilika, bila elimu ni kazi bure hivyo wazazi na walezi wakubali kujinyima mradi kuwapatia watoto wao elimu bora itakayowasaidia maisha yao ya ukubwani," alisema.
Alidokeza katika kuhakikisha shule yao inaendelea kuwapatia watoto elimu bora wanatarajia kuanzisha mtaala wa kimataifa utakaoenda sambamba na ule wa taifa ambao kwa sasa unafundishwa katika shule hiyo.
Nao wageni rasmi wa mahafali hayo, Bushra Maliki na Mchungaji Albert Okanga katika hotuba zao waliwaasa wazazi kujenga uhusiano mzuri na walimu ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na malezi mazuri kwa maisha yao ya baadae.
Bushra ambaye ni Meneja Maendeleo wa Edexcel tawi la Tanzania, alisema amejitolea kushirikiana na uongozi wa shule hiyo ya Joyland ili kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa ngazi ya kimataifa kwa lengo la kuinua elimu nchini na kusaidia watoto wa Tanzania kupata elimu inayostahiki katika dunia ya sasa.
Mchungaji Okanga kwa upande wake alisisitiza kwa kusema ni wazazi wanakijita katika kuwapa watoto huduma vipaumbele kwa ajili ya kuwajengea msingi imara wa maisha kuliko kuwastarehesha, sambamba na kuwa karibu na watoto wao kuwasikiliza kujua matatizo waliyonayo na kuwasaidia kwa haraka.
Katika mahafali hayo wanafunzi waliofanya vizuri mbali na wale wahitimu wa Pre Primary walizawadiwa sambamba na wahitimu wa mafunzo ya lugha ya Kiingereza yanayotolewa bure shuleni hapo kwa lengo la kusaidia ufahamu wa lugha hiyo ya kigeni.

No comments:

Post a Comment