STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 5, 2015

GHARIKA! MVUA ZAUA WATU 42, WENGINE 96 WAJERUHIWA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh14yp-wBksDb2aWv2jU5eXK_DLVeBzzxVVj9B4xyYWtfoly_eXgTWQ8ELZGAP48SidmeqnRD_Biaxg2Bjy9ypcZYYhQuJmjZ2I1xFmTVTu0appX1mnT0Y_bsxNlvKnnRquRUnSSfGXvmA/s1600/kahama+1.jpg
Moja ya nyumba iliyoporomoshwa na mvua zinazoendelea kunyesha
Na Mwandishi Wetu, Kahama
ZAIDI ya watu 40 wameripotiwa kufariki mjini Kahama, Shinyanga kutokana na mvua kubwa huku wengine wapatao 96 wameripotiwa kujeruhiwa na kupoteza makazi.
Aidha mikoa ya Kilimanjaro, Morogoro, Pwani na Tabora mvua kama hizo zenye kuambatana na upepo mkali zimeleta uharibifu mkubwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imeonya huenda mvua hizo za mawe zikaendelea kunyesha mfululizo na watu wawe na tahadhari.
Awali iliripotiwa kuwa 39 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 69 wamejeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kufuatia mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. 
Taarifa hizo zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya amesema mvua hiyo kubwa iliambatana na upepo mkali, hivyo nyumba nyingi zilianguka na nyingine kuezuliwa na kuharibiwa kabisa.
 Bw. Mpesya amesema hadi majira ya asubuhi walikuwa wamefanikiwa kupata miili ya watu 39 waliopoteza maisha baada ya kufukua nyumba nyingi, na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya kwa matibabu zaidi. 
Mkuu huyo wa Wilaya amesema nyumba nyingi zimeanguka na zoezi la kutafuta watu waliojeruhiwa au kupoteza maisha bado linaendelea kwa kasi.
Hata hivyo idadi ya waliopoteza maisha na waliojeruhiwa ilizidi kuongezeka kadri shughuli za uokozi ilipokuwa inaendelea na kuleta simanzi kubwa kwa taifa.

No comments:

Post a Comment