STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 28, 2013

Wawakilishi wa Tanzania Big Brother The Chase hawa hapa

Nando

Feza Kessy
MASHINDANO ya Big Brother Africa ‘Big Brother-The Chase’ yamezinduliwa rasmi juzi nchini Afrika Kusini.
Mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya nane mwaka huu, yanashirikisha jumla ya watu 24 kutoka katika nchi 14 za Afrika.
Washiriki hao wanatarajiwa kukaa ndani ya nyumba hiyo kwa muda wa siku 90 ambapo wataanza kuchujwa kuanzia mwishoni mwa wiki hii.
Tanzania inawakilishwa na Feza Kessy pamoja na Ammy Nando ambapo mshindi wa mwaka huu ataondoka na kitita cha dola za Kimarekani 300,000.
Akizungumza Dar es Salaam juzi wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Habari wa Dstv Tanzania Barbara Kambogi, alisema kuwa pamoja na kuwa msimu huu Ligi mbalimbali zimeshamalizika hivyo mashabiki wengi watapata burudani kupitia katika shindano hilo.
Alisema kuwa mashindano hayo yanaonyeshwa moja kwa moja na Dstv kupitia chaneli 197 na 198 ambapo mashabiki kutoka nchi 50 watapata fursa ya kuyaangalia.
Pia Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Airtel ambao pia ni wadhamini wa mashindano hayo kwa mwaka huu Bw, Levi Nyakundi alisema kuwa mashindano hayo yanazidi kupata umaarufu kutokana na kila mwaka kuwa tofauti.
Aliongeza kuwa wateja wa Airtel wananafasi ya kulipia huduma ya DSTV kwa kupitia huduma ya Airtel kwa kupiga *150*60# kwa urahisi wakiwa nyumbani au sehemu zao za kazi.
“Airtel Money itasaidia sana wateja wetu kuokoa muda wao wa kazi pale wanapolipia huduma ya DSTV wakati wowote wakati wa msimu huu wa Big Brother, mashabiki hawana budi kuwapigia kura washiriki wanaoiwakilisha Tanzania ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi,” alisema Nyakundi.
“Mashindano ya mwaka huu yanaonekana kuwa tofauti na yaliyopita hivyo tunatarajia kupata burudani nzuri na hivyo mashabiki wawapigie kura Watanzania ili wafanye vizuri” alisema.
Katika uzinduzi huo kulikuwa na burudani zilizotolewa na wasanii kutoka Afrika Kusini Mafikizolo pamoja na Stela Mwangi wa Kenya.

No comments:

Post a Comment