STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 27, 2013

Coastal Union kusajili kimyakimya


baadhi ya viongozi wa Coastal Union

WAKATI klabu za Simba na Yanga zikipigana vikumbo na kutambiana kwenye vcyombo vya habari juu ya wachezaji inayowanasa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uongozi wa Coastal Union ya Tanga umesema utafanya usajili wao kimyakimya bila makeke kama vigogo hivyo vya soka nchini.
Coastal iliyorejea kwenye Ligi Kuu msimu wa 2011-2012, imesema kitu cha muhimu na watakachozingatia ni kusajili kwa umakini mkubwa na kwa kiwango cha kimataifa, ili kuiwezesha timu yao kufanya vyema kwa ligi ijayo sambamba na kutimiza malengo waliyojiweka mabyo msimu huu wameshindwa kuyafikia.
Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo, Nassor Binslum, aliiambia MICHARAZO kuwa, hawatafanya usajili wa mbwembwe na makeke badala yake ifanya mambo yao kimyakimya bila kuwashtua watu hadi mwishoni watakapokianika kikosi chao.
Binslum, alisema watakachozingatia ni kusajili wachezaji watakaoiwezesha Coastal ifanye vyema katika ligi hiyo tofauti na msimu huu waliomaliza wakiwa kwenye Sita Bora, kinyume na msimu uliopita walipomaliza nafasi ya Tano.
"Coastal Union hatuna mbwembwe tutafanya usajili wetu kimyakimya na kwa umakini mkubwa ili msimu ujao tutishe na tutakitangaza kikosi mara baada ya mambo yote kukamilika," alisema Binslum.
Mabingwa hao wa zamani wa soka nchini, walimaliza katika nafasi ya sita kwa kujikusanyia pointi 35 kutokana na michezo 26 iliyocheza na ilimaliza msimu vibaya kwa kupewa kichapo cha mabao 2-0 na Polisi Morogoro.

No comments:

Post a Comment