STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 28, 2013

Hussein Javu airuka kimanga Yanga, asisitiza yeye bado wa Mtibwa

Hussein Javu
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar, Hussein Javu ameiruka kimanga klabu ya Yanga kuhusu mipango yao ya kutaka kumsajili kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Javu alisema hajawahi kufanya mazungumzo na kiongozi yeyote wa Yanga na kushangazwa na taarifa kwamba yupo njiani kutua Jangwani akitokea Mtibwa.
Akizungumza na MICHARAZO, Javu alisema mpaka sasa yeye ni mchezaji wa Mtibwa Sugar na angependa kuendelea kuichezea klabu hiyo kwa misimu mingine na hajui wanaomzushia kwamba anajiandaa kuhamia Yanga.
"Sijajua hizi taarifa zinatoka wapi, sijazungumza na kiongozi yeyote wa Yanga kuhusu suala la kuhamia Jangwani, lakini naona naandikwa kuhusu mipango hiyo wengine wakidai nimteoa masharti ya kutaka nyumba na gari," alisema.
Alisema anashukuru kupata nafasi ya kuzungumza na MICHARAZOna kuweka bayana suala hilo ili isije akaeleweka vibaya kwa viongozi na wachezaji wenzake.
Alipoulizwa yupo tayari kutoka Mtibwa Sugar, Javu alisema hajafikiria kwa sasa ila alisema kama kweli kuna klabu inayomhitaji ni lazima izungumze naye pamoja na viongozi wake na wakiafikiana atakuwa na maamuzi sahihi.
"Soka ni ajira yangu, pamoja na kwamba napenda kucheza Mtibwa, kama itatokea klabu yoyote itakayokuwa inanihitaji ikazungumza nami au viongozi wangu naweza kuhama, lakini siyo kwa kuzushiwa kama sasa," alisema Javu.
Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa na bahati za kuzitungua Simba na Yanga kila timu hizo zikikutana na Mtibwa Sugar, alisema ingekuwa vyema vyombo vya habari zinaposikia fununu zozote hasa kipindi hiki cha usajili kikafanya jitihada za kuzungumza na wahusika badala ya kuandika tu na kuharibiana.
Javu amekuwa akihusishwa na mioango ya kutua Yanga kwa nia ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo baada ya washambuliaji waliopo sasa baadhi yao kushindwa kung'ara kwenye msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment