STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, May 17, 2013

Filamu ya Jacklyne Wolper 'My Princess' ipo njiani kutoka

Muonekano wa kava la filamu ya My Princess
FILAMU mpya ya mwanadada anayetingisha nchini katika fani ya uigizaji wa filamu, Jacklyne Wolper iitwayo 'My Princess' inatarajiwa kuachiwa rasmi mwezi ujao baada ya kukwama tangu mwaka jana.
Msemaji wa kampuni ya Papazi Arts and Entertainment Tanzania, Leah Richard 'Lamata' ameiambia MICHARAZO kwamba filamu hiyo iliyotungwa na Wolper na kuicheza yeye pamoja na wakali wengine kama Hemed Suleiman 'PHD' na Emmanuel Simwinga 'Izzo Business' itatoka mapema mwezi Juni.
Lamata alisema maandalizi yote ya filamu hiyo kuachiwa kwa mashabiki yamekamilika na kwamba itasambazwa na kampuni hiyo ya Papazi ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika kuwawezesha wasanii na watayarishaji wa filamu kupitia kazi zao.
"Ile filamu ya Jacklyne Wolper iitwayo 'My Princess' ambayo ilikamilika tangu mwaka jana, lakini ikishindwa kutoka kama ilivyotarajiwa sasa itatolewa rasmi mwezi Juni hivyo mashabiki wakae mkao wa kula kupata burudani," alisema Lamata mmoja wa waongozaji wa filamu wachache wa kike waliopo nchini.
Lamata alisema mbali na filamu hiyo, pia kampuni hiyo pia inatarajiwa kutoa kazi nyingine mpya hata hivyo hakupenda kuzitaja kwa sasa akisisitiza kwanza mashabiki waipokee filamu hiyo.

No comments:

Post a Comment