STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, May 28, 2016

Mascherano, Higuain wajipa tumaini kwa Messi Copa America 2016

http://static.dnaindia.com/sites/default/files/styles/half/public/2016/05/28/465312-messi-injury.jpg?itok=WVjhADzW
Messi akisaidiwa kutoka uwanjani jana Ijumaa alipoumia katika mechi yao ya kirafiki dhidi ya Honduras
HOFU tupu. Kuumia kwa nyota wa Argentina, Lionel Messi kumezua hofu miongoni mwa wachezaji wa timu yake ya taifa inayojiandaa na fainali za michuano ya  Copa America zitakazoanza mwezi ujao nchini Marekani.
Javier Mascherano na Gonzalo Higuain kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakisema kuwa wana matumaini nahodha wao huyo, Lionel Messi atakuwa fiti kabla ya kuanza kwa fainali za Copa America 2016.
Messi aliumia jana Ijumaa katika mechi za kirafiki ya kimataifa dhidi ya Honduras na kusababisha hofu kubwa kwa wachezaji, mashabiki wa Argentina.
Mwanasoka huyo bora wa dunia, alitolewa Uwanjani baada ya kudondoka vibaya na kujiumiza mgongo na mbavu zake kwenye mjini San Juan waliposhinda bao 1-0.
Kocha Mkuu wa Argentina, Gerardo Martino alisema yu tayari kupokea taarifa zozote juu ya majeraha ya Messi, wakiwa wanakabiliwa na mchezo wa ufunguzi dhidi ya watetezi Chile Juni 6.
Hata hivyo mchezaji mwezake wa Barcelona Javier  Mascherano amesema anatumaini Messi atapona haraka na kurejesha Uwanja kwa ajili ya michezo ya Copa America.
Kauli kama hiyo ilitolewa pia na mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo wa Honduras, Gonzalo Hiuguain, alisema anaamini tatizo lililompata nyota wao halitakuwa kubwa kiasi cha kumkosa kwenye michuano hiyo migumu.

No comments:

Post a Comment