STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, June 11, 2013

Bosi Masinde 'kulifufua' kundi la Shirikisho Msanii Afrika


Bosi Masinde katika pozi
MUIGIZAJI mkongwe aliyewahi kutamba na michezo ya kwenye runinga kupitia kituo cha ITV anayekimbiza kwa sasa kwenye filamu, Richard Mshanga 'Bosi Masinde' amesema anafikiria kulifufua upya kundi la Shirikisho Msanii Afrika baada yha kundi hilo kusambaratika kitambo.
Masinde, alisema wazo la kulirejesha upya kundi hilo katika 'uhai' baada ya kuzimika miaka kadhaa iliyopita inatokana na ushawishi anaopata kwa baadhi ya wasanii wenzake wa zamani pamoja na mashabiki ambao walikunwa na maigizo ya kundi hilo wakati likiwa kileleni.
Akizungumza na MICHARAZO, Masinde alisema Shirikisho Msanii Afrika halijafa kimoja, ila liligawanyika pande mbili mara baada ya yeye kujiweka kando na kulifanya kundi hilo lizimike tofauti na iliovyotamba enzi zake likitesa kituo cha ITV.
"Nimekuwa nikiombwa na baadhi ya wasanii nami nafikiria kama nirejeshe majeshi na kulifufua upya kundi hilo ambalo lifukuzana sambamba na Kaole Sanaa kama fitina hazijaingia na kuilisambaratisha," alisema Masinde.
Mshindi huyo wa tuzo ya Muigizaji Bora wa Mwaka wa ZIFF-2012, alisema anajihisi ana wajibu wa kuwarejeshea mashabiki wao burudani kama walivyoipata kupitia michezo kadhaa ilizotamba enzi zao kiasi cha kundi hilo kuwa 'gumzo' la jiji mbali na kuibua nyota kibao.
Enzi za kundi hilo lilitamba na michezo kama 'Tamu Chungu', 'Gumbizi', 'Hatia', 'Dumaza' na mingine huku likiwaibua mastaa wa sasa wa filamu nchini kama akina Amanda, Mama Kawele, Bakar Makuka, Aunty Ezekiel, Nyatawe na wengineo.

No comments:

Post a Comment